Zoezi la kufukua Maiti za watu waliofunikwa na kifusi katika Machimbo
ya Madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi jana
limekamilika leo asubuhi huku wakifanikiwa kuzipata maiti zote 7
Akiongea na mtandao huu,Diwani wa Kata hiyo,Andrew Chikongwe
alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu
kufuatia na kuwepo kwa zana duni za kufukua Mchanga hali iliyofanya
kazi hiyo kuwa Ngumu kuanzia jana saa 9 jioni hadi leo asubuhi
Chikongwe aliwataja Marehemu hao ni Nyang'ana Mkelecha,Mkazi wa
Musoma,Mohamed Omari Fondogoro,Mkazi wa Morogoro,Bakari Liganga mkazi
wa Chunyu Ruangwa,Rajab maarufu ROGER Mkazi wa Musoma,Uwesu Bakari
Abeid mkazi wa Rondo,Chakoda Mkazi wa Dar na Rashid Ally maarufu BADE
Mkazi wa Masasi mkoani Mtwara
kwa hisani ya Abdulaziz video
No comments:
Post a Comment