Thursday, September 13, 2012

Tume ya waziri Nchimbi ya kuchunguza mauwaji ya Mwangosi yaibiwa hotelini

 
Habari kutoka mkoani Iringa zilizoripotiwa na mwandishi  Francis Godwin  Kutoka mjini Iringa zinadai kuwa tume iliyoundwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi kuja kufanya uchunguzi dhidi ya mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoani Iringa na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa, Marehemu Daudi Mwangosi imeibiwa katika hoteli maarufu iliyokuwa imefikia .

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Leo ambapo mmoja Kati ya wajumbe wa tume hiyo ameamka na kujikuta mtupu Basra ya Laptop yake yenye nyaraka nyeti za kumwezesha kufanya uchunguzi huo kuibwa.

Inadaiwa kuwa tume hiyo pamoja na kuundwa na waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya nchi ila bado imekuwa ikifanya kazi katika mazingira hatari zaidi baada ya kuwepo kwa habari kuwa imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu zaidi na makachero wa polisi.

Hat a hivyo habari Kutoka ndani ya jeshi la polisi ambazozinafanyiwa kazi na jeshi la polisi mkoani Iringa zinadai kuwa tume hiyo imeondoka asubuhi hii kuelekea Nyololo kuanza kufanya kazi yake

No comments:

Post a Comment