Al-Shabaab inawateka watoto na kuwalazimisha kuchukua silaha kama sehemu ya jitihada zake za kulinda Jowhar kutofikiwa na vikosi vya Somalia na vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM), wakaazi wameiambia Sabahi.
Watoto wa Somalia, wanakumbana na umaskini na njaa, hususani wako katika uwezekano wa kuathirika kwenye uandikishaji wa wanajeshi kwa mujibu wa sheria za al-Shabaab. Picha iliyo hapo juu inaonyesha watu wakisubiri mgawanyo wa msaada wa chakula katika kambi huko kusini ya Mogadishu wakati wa baa la njaa mwezi Julai 2011 . [Mustafa Abdi/AFP]
Mwanaharakati wa haki za binadamu na watoto Mandeq Mohamed Hassan alisema al-Shabaab inategemea watu vijana kujaza safu zake za maaskari.
"Siwezi kukupa idadi halisi ya watoto wasio na hatia waliondikishwa na al-Qaeda nchini Somalia kwa sababu ni suala gumu sana na la hatari" aliiambia Sabahi . "Ninachoweza kusema, ni kwamba si chini ya asilimia 90 ya askari wote walioandikishwa katika kundi hili ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao wanatoka katika familia zinazokumbwa na umaskini na koo ndogo ambazo kisiasa hazina uwakilishi."
No comments:
Post a Comment