Wednesday, September 12, 2012

MALEMA AITISHA MGOMO WA KITAIFA WA WACHIMBA MIGODI


Mwanaharakati wa kisiasa nchini Afrika Kusini Julius Malema ametoa wito wa maandamano makubwa ya kitaifa nchini humo kwa wafanyakazi wa migodini.
"wamekuwa wakiiba madini haya ya dhahabu kutoka kwenu." bwana Malema aliambia wachimba migodi waliokuwa wanamshangilia katika mgodi mmoja wa dhahabu mashariki mwa Johannesburg.
"sasa ni wakati wenu." aliongeza Malema.
Migomo migodi ya wachimba migodi imekumba Afrika Kusini na kuathri shughuli za kuchimba madini ya Platinum na dhahabu katika nchi hiyo yenye rasilimali nyingi.
Lakini baadhi wanamtuhumu Malema kwa kuwa na njama na kujinufaisha kisiasa huku wengi wakiwa bado wanaomboleza vifo vya wachimba migodi 34 wa Marikana mwezi jana nchini humo.
Watu 44 walifariki katika mgodi huo katikati ya mwezi Agosti. 34 wakipigwa risasi na kuuawa na polisi kwa siku moja.

No comments:

Post a Comment