Tuesday, September 25, 2012

MIKOBA YA KANUMBA SASA YARISIWA NA SETH BOSCO


MSANII Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na msanii nyota aliyetikisa tasnia ya filamu nchini marehemu Steven Kanumba amekusudi kufunika pengo liloachwa na marehemu kaka yake akiongea na Mwanaspoti msanii huyo amesema katika kumuenzi kaka yake ni kuhakikisha kuwa kampuni inaendelea na kufanya kazi za filamu zenye nzuri na ubora.

Seth Bosco akiongea na vyombo vya Habari havipo pichani

Filamu ya Malaika filamu ya kwanza akiwa kinara


“Baada ya kumaliza msiba na taratibu zingine kampuni ya Kanumba Great Film inaendelea na kazi zake kama awali na kufanya katika ufanisi wa hali ya juu, nakumbuka hosia wake juu yangu na kwa kufuata hayo namuenzi kwa kutengeneza filamu ya Malaika ambayo mimi ni mhusika,”anasema Seth.

Seth licha ya kuwa ni mdogo wake na marehemu lakini pia ndio aliyekuwa mtu wa karibu na marehemu Kanumba, katika filamu hiyo ya Malaika Seth anaigiza na mwanadada Rose Ndauka ambaye pia aliwahi kufanya kazi na marehemu, wasanii wengine wanaoshiriki katika filamu hiyo ni Abdalah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’, Maya na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment