Monday, September 10, 2012

WASIFU WA RAISI MPYA WA SOMALIA


Hassan Sheikh Mohamud

Baada ya takriban miaka 21 tangu alipouwawa Rais wa nchi hiyo Marehemu Said Bare, Hatimaye wabunge wa nchi hiyo leo wanafanya uchaguzi wa kumpata Rais wao ndani ya Somalia, hii ni baada ya majaribio kadhaa ya kufanya uchaguzi wa Rais wakiwa nje ya Somalia na nchi kushinwa kutawalika na wa - Somali kuendekeza uchaguzi wa viongozi wao kutokana na ukabila, vikundi na koo na kuwa nchi yenye mauaji na maharamia kama El Shabab na wengine

Hassan Sheikh Mohamud ni mwanataaluma, mwanasiasa na mwanaharaki wa kiraia aliyewahi kufanya kazi katika mashirika kadhaa ya kitaifa na kimataifa ya amani na maendeleo.

Mohamud alihitimu katika Chuo Kikuu cha Taifa cha somalia mwaka 1981 na kwenda kusoma India ambako alipata shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Bhopal mwaka 1988.

Mwaka 1993, Mohamud alifanya kazi katika Mfuko wa Dharura wa Watoto wa Umoja wa Mataifa kama afisa wa elimu kusini na kati ya Somalia mpaka kuondoka kwa Operesheni ya Umoja wa Mataifa katika vikosi vya Somalia mwaka 1995.

Mwaka 1999, alishiriki katika kuanzisha Taasisi ya Somalia ya Uendeshaji na Maendeleo ya Utawala, ambayo baadaye iligeuka kuwa Chuo Kikuu cha Simad, ambako alikuwa mkuu wa chuo hadi mwaka 2010.

Mwaka 2011, alianzisha Chama cha Amani na Maendeleo na hadi sasa ndiye mwenyekiti wake.

Mohamud anazungumza Kisomali na Kiingereza.

No comments:

Post a Comment