.jpg)
Matokeo yalionyesha kwamba kazi za ubongo wa wazee katika kundi ambalo lilikuwa linatumia mtandao mara kwa mara ziliimarika zaidi kuliko za wazee katika kundi ambalo halikutumia mtandao. Mabadiliko makubwa yalionekana katika sehemu za ubongo zinazoshughulika na kumbukumbu (memory), lugha, kusoma na upambanuzi.
Matokeo haya yamewafurahisha wanasayansi na wanasema kwamba pengine matumizi ya mtandao yanaweza kuwa silaha mojawapo dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na upotevu wa kumbukumbu na utambuzi kama vile Alzheimer.

Sina uhakika kama kweli wazee wa Kiafrika wanahitaji mtandao kuimarisha kazi za ubongo wao. Mimi nadhani kwamba michezo kama vile bao, drafti na hata kuhesabu ng’ombe wanaporudi nyumbani kila jioni ni mazoezi tosha yanayoweza kusisimua kazi za ubongo, mazoezi ambayo yamesaidia kuwafanya wazee wengi wa Kiafrika kubakia makini kiutambuzi (cognitively) hata katika umri mkubwa. Sijui kama tulikuwa na wagonjwa wengi wa Alzmeimer barani Afrika kabla ya hili wimbi jipya la utandawazi tunaolishuhudia kwa sasa.