
Watu wanaotumia email za Gmail, Hotmail na Yahoo wanashauriwa kubadili password zao haraka iwezekanavyo baada ya watu wasiojulikana kuhack maelfu ya email za watu na kisha kuziweka hadharani kwenye mitandao.
Awali siku chache zilizopita watumiaji wa email za Hotmail walishauriwa kubadili password zao baada ya watu wasiojulikana kuzihack email 10,000 za Hotmail na password zake na kisha kuziweka kwenye website ya Pastebin.com ambayo wataalamu wa kutengeneza website toka kona mbali mbali duniani humegeana ujuzi walio nao.
Wakati Microsoft ikiwashauri watumiaji wa Hotmail wabadili password zao, orodha nyingine ya email 30,000 za Yahoo, Gmail, AOL, Comcast na Earthlink pamoja na password zake imesambazwa kwenye mitandao duniani.
Ukiachilia mbali email hizo 40,000 ambazo ziliwekwa kwenye internet, haijajulikana ni watu wangapi watakuwa wameibiwa email na password zao hadi sasa.Email hizo ziliibwa baada ya wezi wa email hizo kutengeneza website feki zinazofanana na Yahoo, Hotmail, Gmail n.k ili kuwachuuza watu waandike email na password zao wakidhania wanaingiza kwenye tovuti husika kumbe ndio wanawapa mikononi wezi hao email na password zao.
Staili hiyo ya wizi hujulikana kama "Phishing" na browser nyingi mpya kama vile internet Explorer 7 na Mozilla FireFox zina programu ndani yake kwaajili ya kukulinda na wizi kwa njia ya "Phishing".
Hofu kubwa ni kwamba wahalifu wa kwenye mitandao wanaweza wakatumia email hizo kuiba vielelezo muhimu vinavyohitajika kwaajili ya akaunti za benki na credit card.Kwa mfano fikiria mtu akishapata email na password yako ataweza kujua majina yako kamili na tarehe yako ya kuzaliwa vitu ambavyo anaweza akavitumia kukamilisha wizi wake.
Pia kama utakuwa umehifadhi kwenye email yako au uliwahi kumtumia mtu email yenye vielelezo vyako vya benki na hukuifuta basi wezi hao wa mitandao kazi yao itakuwa imerahisishwa zaidi.Yahoo, Gmail na Hotmail wamewashauri watumiaji wa email zao wawe na tabia ya kubadilisha password zao kila baada ya siku 90.
No comments:
Post a Comment