Kuna raha kubwa kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia mpya za mawasiliano kwa uhuru bila woga au kizuizi chochote. Ziko nchi ambazo uhuru huu ni ndoto. Ndio maana kukawa na mradi wa Global Voices Advocacy (www.http://advocacy.globalvoicesonline.org/) ambao kazi yake ni kutetea uhuru wa kujieleza mtandaoni bila woga. Wakati tuko sisi tunaoweza kujieleza bila woga mtandaoni, wako wenzetu ambao wakifungua mdomo tu kukosoa wezi wenye vyeo kama rais, waziri mkuu, na wengine, basi jela itawaita. Kwa sababu hii, ninaupenda mradi huu na ninaupigia kura. Kura hii inaweza kusaidia mradi huu kupata dola 3,000 za Kimarekani. Kura yenyewe inapigwa kwa kuandika kuhusu GV Advocacy.
Hata wewe kama unaupenda unaweza kuupigia kura kwa kuandika kwenye blogu yako kama nilivyoandika. Maelezo yenyewe utayapata kwenye anuani hii: http://www.zemanta.com/bloggingforacause/
No comments:
Post a Comment