
Saturday, December 25, 2010
Weakleaks Yaihusisha Tanzania Na Uranium DRC
BAADA ya tovuti inayovujisha siri nyeti za Serikali za nchi mbalimbali duniani kuanika siri za Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mtandao huo wa WeakLeaks umefichua siri nyingine nzito kudai kuwa Tanzania ni kitovu cha
usafirishaji madini ya uranium kwenda nchini Iran
Kwa mujibu wa taarifa za tovuti hiyo, Marekani inazishutumu nchi mbili katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania kwa kwa madai ya kuwa kitovu cha usafirishaji kinyemela madini hayo hatari.
WeakLeakes ambao ulifichua siri mbalimbali za Balozi za Marekani, unaitaja Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuwa ndilo chimbuko la madini hayo ambayo baada ya kusafishwa hutumika kutengeneza nguvu ya umeme na silaha hatari.
Ilidaiwa kuwa madini hayo ya uranium yanachimbwa na kampuni za kigeni katika Jimbo la Katanga kabla ya kampuni hizo kuyasafirisha kwenda Iran kupitia ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika taarifa za mtandao huo, mwanadiplomasia wa Marekani jijini Dar es Salaam, Purnell Delly Septemba 2006 anadaiwa kuripoti kwa wakuu wake mjini Washington akisema inafahamika wazi meli zilizosheheni madini ya uranium zimekuwa zikipita katika bandari ya Dar es Salaam zikiwa njiani kwenda Iran.
Kutokana na taarifa hiyo miaka miwili baadaye Polisi wa Kenya waliamua kuingilia kati kile walichohisi, Uganda kusafirisha madini hayo kutoka DRC na kufanikiwa kukamata vifaa hatari vya milipuko na kutiwa mbaroni wanaume wawili waliodaiwa kununu vitu hivyo kutoka DRC kwa thamani ya sh. milioni 3.9 na walipanga kuviuza mjini Nairobi kwa thamani ya sh. milioni Sh.100.
Mei mwaka huu, Polisi nchini Kenya walifanikiwa kukamata kilo 10 ya vitu vinavyosadikika kuwa ni madini ya uranium, hali ambayo ilizua taharuki kwa Jumuiya za Kimataifa kwamba nchi hiyo ilikuwa ikitumika kama njia ya kusafirishia madini hayo kutoka DRC.
Mtandao huo pia ulimnukuu Balozi wa Uswiss akidai kuwa Afrika Mashariki ndiyo njia kuu ya kusafisha madini ya Uranium.
“Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mwandamizi wa Uswiss, usafirishaji wa uranium kupitia bandari ya Dar es Salaam unafahamika bayana kati ya kampuni mbili za meli kutoka Uswiss,” aliandika Delly.
“Hans Peter Schoni,ambaye ni Balozi wa Uswiss nchini Tanzania, alishazungumzia kuhusu tuhuma za madini ya uranium kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kupitishwa katika nchi za Zambia na Tanzania kwenda Iran, lakini hakupewa jibu lolote kutoka kwa kampuni husika ama mahali panapodaiwa kupelekwa madini hayo,”aliongeza mwanadipolimasia huyo.
Alielezea kusikitishwa kwake pamoja na taasisi husika lakini haijawahi kuthibitishwa ama kukanushwa ripoti hizo kuhusu meli hizo za uranium.
Katika ripoti hiyo, Delly ana wasiwasi kwamba huenda mwanadiplomasia wa Marekani mjini Kinshasa, Dpopovich Econoff, ambaye tovuti hiyo ya siri ilimtaja Novemba mwaka 2007 akisema kuwa kuna madini mengi ya uranium nchini DRC.
“Haifahamiki wazi kama kampuni ya Malta Forest ama kampuni nyinginezo zilizopo katika Jimbo la Katanga zinahusika na usafirishaji wa uranium. Mazingira ya kuwepo kwa biashara hiyo yanaonekana lakini ushahidi wa uhakika ndiyo hauonekani,”aliripoti Econoff na kuongeza;
“Vilevile kuna faida kubwa kutokana na kiwango cha uranium kinachozalishwa na kampuni ya Malta Forest's Mines hususani tangu bei ya madini hayo ilipopanda kutoka wastani wa dola 15 mwaka 2004 na kufikia wastani wa dola 135 kwa paundi mwaka 2007,”
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo madini hayo yanachimbwa kwa wingi na kampuni zinazomilikiwa na vigogo ndani ya Serikali ya DRC na kusafirishwa nje ya nchi kwa njia ya panya na mitandao ya rushwa.
Alisema mfano kampuni ya Malta Forest inahusishwa na mshauri wa Rais Joseph Kabila huku kampuni za Uswiss na Finnland zikijipatia faida kubwa kutokana na madini hayo katika Jimbo la Katanga. Chanzo, gazeti Majira
Thursday, December 2, 2010
SOKO KUU LA UHINDINI JIJINI MBEYA LA TEKETEA KWA MOTO
Wafanya biashara wakijaribu kuokoa mali zao kutoka madukani mwao
Umati mkubwa ulio jitokeza kushuhudio tukio la moto
Wafanya biashara wakikusanya vitu vidogovidogo vilivyo salia katika maduka yao
Moto ukiendelea kuteketeza soko kuu la uhindini
Wanahabari kutoka jijini Mbeya waki muhoji mmoja kati ya askari wa kikosi cha zima moto
Gari la kikosi cha zima moto likifika katika eneo la tukio kwa kuchelewa na baada ya muda kidogo kuondoka kwenda kujaza maji kwa madai kuwa maji yamekwisha
Tuesday, November 2, 2010
MHESHIMIWA SUGU ATANGAZWA RASMI KUWA MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA MJINI
waandishi wa habari mbalimbali waki fanya mahojiano na
mheshimiwa SUGU baada ya kutangazwa mshindi
Hapa zoezi la kumtangaza mshindi likiendelea ndani ya chumba cha kuhesabia kura
Mr II akibadilishana mawazo na Mkoloni ambaye pia alikuyepo kusimamia kura za SUGU Jijini Mbeya
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini aki pongezwa na viongozi pamoja na marafiki
Akina dada hawa ni makamanda wa CHADEMA ambao wamekuwa wakitupatia support ya kutosha na sasa wakilia kwa furaha iliyoje baada ya NEC kumtangaza SUGU kuwa Mbunge mpya wa Meya Mjini
Wednesday, October 13, 2010
Book Thrown at President Obama
No publicity is bad publicity. If you subscribe to that philosophy, either your name is Michael Lohan, or you think throwing a book at the President is a smart move. At a weekend rally in Philadelphia, the Secret Service detained an author and "overly exuberant" Barack Obama supporter who wanted to share his work with him. By winging a paperback copy at his head. The determined scribe said he meant no harm but exercised horrendous judgment, and was later released without being charged. Check out the ambush below ...
Gari linalojiendesha lenyewe kutoka google company
kampuni ya google imetengeneza gari linalojiendesha lenyewe ambalo haliitaji driver, unakumbuka movie ya mwaka 1993 ya sylvester stallone na wisley snipes ya demoliton man, inasemekana gari hizi zitakapoingia sokoni zitapunguza ajali za barabarani zinazosababisha vifo na ulemavu kwa watu kila siku
Friday, October 8, 2010
Tukiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Tanzania ambao utafanyika October 31, 2010
Watanzania wazalendo wanachama na wapenzi wa Chadema mnaombwa kuchangia kwa dhati harakati za Chadema ili tuweze kuwafikia Wananchi wengi zaidi katika kila kona ya Tanzania tukitafuta ridhaa yenu ya kuweza kujenga nchi yetu; nchi yenye usawa, uzalendo, maadili na uwajibikaji katika miaka mitano ijayo.
CHANGIA CHADEMA KUPITIA BANK:
CRDB BANK
CHADEMA - M4C
Account Number: 0J1080100600
National Microfinance Bank [NMB]
CHADEMA
Account Number: 2266600140
Unaweza kuweka pesa kupitia tawi lolote la Benki hizi Tanzania.
CHANGIA CHADEMA KUPITIA SMS (MESEJI):
Tuma neno:
"CHADEMA" kwenda namba 15710
"NAJIUNGA" kwenda namba 15710
"SLAA" kwenda namba 15710
Unaweza kutuma meseji mara nyingi kadri unavyoweza na kila ujumbe utagharimu TZS 350/= tu.
HII NI KWA MITANDAO YA ZAIN, TIGO NA VODACOM TU.
CHANGIA KUPITIA M-PESA:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa M-Pesa wanaweza kutumia namba zifuatazo:
0758 223 344
0764 776 673
CHANGIA KUPITIA ZAP:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa ZAP wanaweza kutumia namba hii:
0789 555 333
"Ndugu Zangu Watanzania, tunawaomba kwa dhati kabisa tushikamane, tushirikiane bila kujali itikadi zetu kuchangia harakati hizi, tunawashukuru sana. - Dr. Wilbroad Peter Slaa"
CHAGUA MABADILIKO YA KWELI. CHAGUA CHADEMA.
CHANGIA CHADEMA KUPITIA BANK:
CRDB BANK
CHADEMA - M4C
Account Number: 0J1080100600
National Microfinance Bank [NMB]
CHADEMA
Account Number: 2266600140
Unaweza kuweka pesa kupitia tawi lolote la Benki hizi Tanzania.
CHANGIA CHADEMA KUPITIA SMS (MESEJI):
Tuma neno:
"CHADEMA" kwenda namba 15710
"NAJIUNGA" kwenda namba 15710
"SLAA" kwenda namba 15710
Unaweza kutuma meseji mara nyingi kadri unavyoweza na kila ujumbe utagharimu TZS 350/= tu.
HII NI KWA MITANDAO YA ZAIN, TIGO NA VODACOM TU.
CHANGIA KUPITIA M-PESA:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa M-Pesa wanaweza kutumia namba zifuatazo:
0758 223 344
0764 776 673
CHANGIA KUPITIA ZAP:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa ZAP wanaweza kutumia namba hii:
0789 555 333
"Ndugu Zangu Watanzania, tunawaomba kwa dhati kabisa tushikamane, tushirikiane bila kujali itikadi zetu kuchangia harakati hizi, tunawashukuru sana. - Dr. Wilbroad Peter Slaa"
CHAGUA MABADILIKO YA KWELI. CHAGUA CHADEMA.
Saturday, September 18, 2010
Wednesday, September 15, 2010
BOW WOW MADE IN CHINA AKA BOW WOW FAKEY AZAMA NDANI YA TUZO ZA MTV VMAS BILA KUSHTUKIWA
MAREKANI INASIFIKA KWA VITU VINGI NA MOJA WAPO NI UMAKINI WA WAANDAAJI WA TUZO MBALI MBALI KATIKA SWALA LA USALAMA BT WEEKEND HII UMAKINI HUO ULIONEKANA UPO KWENYE SHAKA SHAKA BAADA YA BOW WOW FEKY KUZAMAA NDANI YA PRE SHOW YA MTV VMA, SHOW AMBAYO DOGO JUSTINE BIEBER, AMBAE BAADAE ALIKSHINDA TUZO YA MSANII BORA CHIPKIZI, ALIKUW ANATUMBUIZA
BOW WOW HUYO FAKY ALIWEZA KUINGIA NDANI YA UKUMBI HUO WA NOKIA PANDE ZA LOS ANGELES KWA MSAADA WA WALINZI WA TUZO HIZO NA ALIWEZA KUFANIKIWA KUPIGA PICHA NA MAFANS KABLA YA KUINGIA UKUMBINI
BOW WOW HUYO FAKY ALIWEZA KUINGIA NDANI YA UKUMBI HUO WA NOKIA PANDE ZA LOS ANGELES KWA MSAADA WA WALINZI WA TUZO HIZO NA ALIWEZA KUFANIKIWA KUPIGA PICHA NA MAFANS KABLA YA KUINGIA UKUMBINI
YOTE HAYA YALIWEZEKANA KWA KUWA BOW WOW ORIGINAL HAKUHUDHURIA TUZO HIZO KWA SABABU AMBAZO HAZIKUWEKWA WAZI?!
ZAMA KWENYE SURA KITABU AKA FACEBOOK KATIKA UKURASA WA EXTRA EXTRA LARGE NA UCHEKI PICHA YA BOW WOW HUYO FAKEY NA UNIAMBIE KAMA INGEKUWA WEWE, ANAGEFANIKIWA KUKUPIGA CHANGA LA EYES
Tuesday, September 14, 2010
KEISHA AJITOA TIP TOP CONNECTION
MANAGER WA KUNDI LA tIP TOP cONNECTION, MAARUFU KAMA BABU TALE LEO (13/09/2010) AMETHIBITISHA KUTOKA KWA MWANADADA KEISHA ALIYEKUA KATIKA KUNDI HILO KWA MUDA MREFU SASA. Awali taarifa zilianza kuenea mtaani baada ya keisha kufanya mahojiano na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amejitoa kutokana na manager wa kundi yaani babu tale hasimamii vizuri kazi zake.
Babu tale amesema, keisha ameomba kujitoa na kundi likamruhusu aondoke, na kundi lao halito athirika kwa mwanadada huyo kuondoka kwani hiyo si mara ya kwanza, aliwahi kuondoka na akarudi mwenyewe kundini.
miongoni mwa wasani waliowahi kuondoka katika kundi kwa sababu tofauti tofauti moja wapo ikiwa ni madai ya kudhulumiwa mikwanja ni MB-dog, z-anto na sasa hivi keisha.
Monday, September 13, 2010
Will and Jada Smith’s daughter gets a record deal with Jay-Z, Debuts first Single!!
Willow Smith, the 9-year-old daughter of Hollywood Power Couple Will and Jada Pinkett Smith, is poised to make her debut as a recording artist after inking a deal with hip-hop mogul Jay-Z’s Roc Nation label.
Willow has made it clear that she’d like to follow the footsteps of her famous parents and brother Jaden
Her first song — an uptempo club banger titled “Whip My Hair” — hit the Interwebs this week, and a video for the single will be shot in Los Angeles later this month.
Jay-Z, who appeared alongside his new protege on Ryan Seacrest’s KIIS-FM radio show Thursday (CLICK HERE For AUDIO), says it’s rare to find an artist with such talent and creativity at Willow’s tender age. In fact, Willow’s sing-song vocals already have the pint-sized stylista drawing comparisons to another of Hov’s mohawked signees: “Rude Boy” singer Rihanna.
“We at Roc Nation are excited to work with Willow. She has an energy and enthusiasm about her music that is truly infectious. It’s rare to find an artist with such innate talent and creativity at such a young age. Willow is about to embark on an incredible journey and we look forward to joining her as she grows in all aspects of her career.”
Willow, whose dad Will was the first rapper to win a Grammy award, is ecstatic about carving out a place for herself in the music world.
Saturday, September 11, 2010
Tazama Blog hii mpya ya Mr II (SUGU)
Hebu jaribu kutazama blog hiii mpya inayo julikana kwa jina la Sugu For Mbeya kupitia adress hii www.suguformbeya.blogspot.com
Monday, September 6, 2010
Sikiliza ngoma exclusive Audio: My Time – Diva’s Swagger feat. Ben Pol
Song: My Time feat. Ben Pol
Artist: (Divas Swagger)Teklah Nendeze, Vanessa, Angeris, Chiku K, Linah, Baby J, Aneth, Mary Lucas, Pipi
Producer: Duke
Studio: Music Lab
2010.
for time unaisikia hapa
Artist: (Divas Swagger)Teklah Nendeze, Vanessa, Angeris, Chiku K, Linah, Baby J, Aneth, Mary Lucas, Pipi
Producer: Duke
Studio: Music Lab
2010.
for time unaisikia hapa
Saturday, September 4, 2010
RESPECT MY VOTE
Kiukweli ni Tshirt nzuri na zilizo beba ujumbe ikionyesha ni jinsi gani wa Tanzania tume zinduka kutoka usingizini na kutaka kutumia kura zetu kuchagua vioongozi waleta maendeleo .
Kwa mahitaji ya Tshirt hizi za respect my vote hebu wasiliana nasi kwa namba 0655785544 au kwa mail hii hapa dannycmfu@gmail.com . nyote mnakalibishwa kwa tshirt zenye ubora na kiwango cha kimataifa .
Kwa mahitaji ya Tshirt hizi za respect my vote hebu wasiliana nasi kwa namba 0655785544 au kwa mail hii hapa dannycmfu@gmail.com . nyote mnakalibishwa kwa tshirt zenye ubora na kiwango cha kimataifa .
Wednesday, September 1, 2010
HAYA NDIO MAISHA BORA ALIYO TU AHIDI MWESHIMIWA
Kiukweli kama mtu una fukia hatua ya kuvaa ngua miaka mitano tena , na nguo yenyewe ni aliyo pewa wakati wa kampeni za mwaka 2005 mpaka leo hii 2010 kwenye kampeni nyingine tuna hitaji kuji uliza mara mbili mbili . huyu bibi nili mkuta maeneo ya SAE loe aki kata majani kwaajili ya ng'ombe wake .
Leo nili tembelea studio ya South Side Records
Studio ndani mambo yaki endelea kupikwa
Drum machine
Huyu ndie mmiliki wa studio hiii mpya pande hizi za mbeya anajulikana kwa jina AGREY KABUJE
Drum machine
Huyu ndie mmiliki wa studio hiii mpya pande hizi za mbeya anajulikana kwa jina AGREY KABUJE
Saturday, August 21, 2010
KIKWETE 2010 OFFICIAL SITE.
Habari zenu Ndugu wapendwa,
Tunayofuraha kubwa kuwafahamisha ya kwamba tovuti maalumu na rasmi ya Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. M. Gharib Bilal sasa inapatikana kwenye mitandao:
www.kikwete2010.co.tz
Tembelea tovuti hii maalumu ya Mgombea Uraisi na Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM mwaka 2010 upate habari mbalimbali kama:
Wasifu wa Wagombea – Mhe. Jakaya M. Kikwete na Dr. Mohammed Gharib Bilal.
· Mafanikio katika sekta mbalimbali.
· Sera na Malengo 2010 – 2015.
· Ratiba za kampeni.
· Hotuba maalumu.
· Matoleo ya Habari.
· Video na picha.
· Mitandao ya Facebook,Twitter na Youtube.
Kupitia tovuti hii na mitandao yake utaweza kupata taarifa mbalimbali na kutoa maoni yako.
“ PAMOJA TUZIDI KUSONGA MBELE”
KICHWA KINGINE KINACHOTUWAKILISHA KWENYE TUNZO ZA CHANNEL O
Anajulikana kwa jina la Gelly wa Rhymes na yeye yupo katika kundi hili katika tunzo za Channel O video music Awards
MOST GIFTED RNB
JON GERMAIN – IN MY HEAD
TOLUMIDE – MY LOVE
GELLY – MZURI
URBAN REIGN – ADDICTED
ANSELMO RALPH – DOMESTICADO
MOST GIFTED RNB
JON GERMAIN – IN MY HEAD
TOLUMIDE – MY LOVE
GELLY – MZURI
URBAN REIGN – ADDICTED
ANSELMO RALPH – DOMESTICADO
Thursday, August 19, 2010
HAPPY B,DAY ALLI TALL. (AT)
Tarehe ya leo 19/8 ni tarehe niliojia duniani AT na Baba mzazi wangu na Dada wangu Mungu Tujalie kila la kheir na Maisha mema marefu yenye Fanaqa na Upendo kwakila mtu Enshallah Amin....
pia Hppy BrthDay wenzangu mlio zaliwa 19/8
Thursday, August 5, 2010
Huyu ndio LORD CASH
Baada ya kimya kilefu katika mzuki kijana Lord Cash anataraji kuja na ngoma zake mpya zilizo tengenezwa kwa ubora mkubwa na kudaikuwa sasa ndio wakati wake kushine
Wednesday, August 4, 2010
Saturday, July 31, 2010
CHRISS TUCKER ANAUZA JUMBA LAKE KWA BEI CHEE
Kuna ripoti zimetufikia kwamba super star aliyetisha katika movie kibao kama RUSH HOUR 1 2 na 3, pamoja na FRIDAY Actor Chriss Tucker anajaribu kulazimisha kuuza Jumba lake la kifahari alilolinunua miaka mitatu iliyopita, Inavyoonekana jamaa alitangaza dau kubwa, Ma Don wa kiwanja wakampotezea jumba hilo alili… Continue
Kanye at FB - "Chain Heavy"/Freestyle?
Siku ya jumanne Rapper kanye West alitokeza makao makuu ya facebook nchini marekani na Kuperform mbele ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, Jamaa alikuwa katupia Suti nyeusi, show hiyo inavyoonekana haikuwa Rasmi kiviile koz hakukuwa na stage, so kanye alipanda juu ya meza za ofisi hiyo na Kuperform ngoma zake mpya zinazohisiwa zitakuwemo katika album yake anayoipika ndani ya mji wa Hawaii, Wachambuzi wa maasuala ya muziki wanasema huenda hatua hiyo ya Kanye west Kuperform mbe… Continue
Thursday, July 29, 2010
Wednesday, July 28, 2010
"HUU NI WARAKA WANGU KWA WASANII WA MZIKI KABLA YA UCHAGUZI MWEZI OCTOBER"
Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi october mwaka 2010,huu ni waraka wangu kwa wasanii wote wa mziki wa kibongo!. Najua kuna miaka mingi sana ya kuukomboa huu mziki wetu lakini wazungu wanasema "One step at a time"...na muda ndio huuu..........!!!!
Miaka kibaao sasa wasanii mmekuwa mkilalamika juu ya kudhulumiwa haki zenu kwa kuibiwa kazi zenu na kulipwa malipo madogo ya album zenu kiwango kisichokidhi mahitaji yenu,hilo ni sawa kabisaaa!!
LAKINI je!! mmejipanga vp kumaliza hili tatizo lenu? kila kukicha viongozi wanawa-ahidi kwa mdomo kuwa watamaliza tatizo lenu bila utekelezaji wa vitendo kitu ambacho mimi nakiona kama ni kiini macho na nyinyi wenyewe mnakifahamu....
Viongozi hawa hawa ambao wanakataa kwa "makusudi" kusimamia maslahi yenu ndio hao hao wanaokuwa wa kwanza kuwachukua nyinyi wakati wa uchaguzi ili muwasaidie kuwapigia kampeni kwa kutoa burudani pindi wanapokuwa kwenye mikutano yao,,,,
Sasa inakuwaje mnatumika kirahisi namna hii? wakati kwenye interview zenu wengi wenu mnajinadi kuwa nyinyi ni wanaharakati na sasa mnafanya mageuzi ya huu mziki wenu,vp mageuzi ndio haya? Mnapotumiwa kwenye kampeni mnacheka cheka kwa furaha pale mnapopewa laki kadhaa au vimilioni kama shukrani ya "kinafki" kutoka kwa hao watu waliowatumia!!!! Na baada ya kumaliza kampeni zao hao hao wakiwa madarakani wanawasahau na kujifanya hawawakumbuki tena hadi wakati mwingine wa uchaguzi.....(huu ni utumwa wa kifikra) najua mtasema mnaangalia pesa na ndio mana mnawafanyia kazi yao na sio kitu kingine!!! Sawa sikatai huenda ni kweli pesa ndio mnayofuata,,, sasa je? nyie wasanii wa kiume ikitokea wamama wakiwapa pesa za kutosha na kuwataka mkatumbuize kwenye "kitchen party" yao mtaenda kudhalilishwa sababu ya pesa au mtakataa?
Sidhani kama ntapata dhambi nikisema kuwa kitendo cha wasanii kutumiwa kwa muda na hawa watu mi nakifananisha na binti wa kike ambae bwana wake huwa anajifanya kumjali na kumfuata pale anapotaka penzi lake tu!! na akishamaliza shida zake anaondoka na kumuacha binti huyo akiteseka na hali ngumu ya maisha bila ya msaada wowote na hurudi tena pale anapokuwa na shida hiyo!!
Enyi wasanii kwanini mnajipa thamani ndogo kiasi hicho???
Huu ndio wakati wenu wasanii kuonesha mapinduzi yenu na misimamo yenu na zile harakati ambazo kila kukicha mmekuwa mkizitaja kwenye nyimbo zenu na interview zenu,,,yawapasa kudai maslahi yenu kwanza kuliko kutumika kuhangaikia maslahi ya watu wengine....
Sitoona ajabu nikiwaona wasanii wale wale wanaokuwa wa kwanza siku zote kudai haki zao wakitumika kwenye kampeni mwezi october na kisha baada ya uchaguzi mwakani wasanii hao hao tutawaskia tena wakilalamika kutokumbukwa na viongozi husika!!!
"CALCULATE THE RISK,BEFORE YOU JUMP"
Sunday, July 25, 2010
Fataki............ Umewahi kujiuliza haya?
atika kuwalinda wasichana dhidi ya KUDANGANYIKA na KUHARIBU NDOTO ZA MAISHA YAO... kuna matangazo kadhaa yanatoka kwenye redio na TV kuhusu "FATAKI".Hivi ndugu zanguni, pamoja na nia njema kabisa ya kutetea haki za watoto wa kike, mmeshawahi kujiuliza athari wazipatazo wakina kaka, baba wenye majina ya FATAKI, na vile vile watoto ambao baba zao wana majina ya FATAKI? Leo nilisikia kisa cha mtoto aliyetaka baba yake anayeitwa FATAKI abadili jina maana shuleni watoto wenzie wanamcheka! Baba naye akajaribu kumshari mwanae kuwa jina hilo lina historia ndefu sana katika ukoo na hawezi kubadili! Nikajiuliza, huyu mtoto naye si ana haki zake? Huko shule kama anataniwa ni dhahiri kuwa anapoteza kujiamini, ana athirika kisaikolojia na hatimaye athari hizi zina uwezekano kum haribia ndoto zake za maisha bora huko mbeleni.
Kwa haraka haraka, nikasema hili linahitaji mjadala mrefu ili kudadavua yaliyomo kama yamo ninavyoyaona mimi.
Karibuni tujadili ili tuwalinde wenye majina ya FATAKI na kutetea haki zao.
Kwa haraka haraka, nikasema hili linahitaji mjadala mrefu ili kudadavua yaliyomo kama yamo ninavyoyaona mimi.
Karibuni tujadili ili tuwalinde wenye majina ya FATAKI na kutetea haki zao.
Mbunge mtarajiwa kupitia Chadema aliyenaswa na mguu wa mtu aliza makanisa
Baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali mkoani hapa, wako katika kilio kufuatia kitendo cha mgombea Ubunge wa Chadema aliyerudisha fomu, George Mtasha (50) kudakwa na jeshi la Polisi wilayani Chunya akiwa na mguu wa kushoto wa binadamu, Risasi Jumamosi linashuka kikamilifu.
Wakiongea na Mwandishi Wetu, baadhi ya waumini hao walisema kuwa, wanaamini kitendo hicho ni ishara ya mwanzo wa vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikiukumba mkoa wa Mbeya miaka ya karibuni.
Josephat Mwaibabile ambaye ni Mzee wa Kanisa la Kiroho la Jerusalem Temple, alisema kuwa mkoa wa Mbeya una skendo ya watu kuchunwa ngozi, waumini wakalia kwa Mungu kwa maombi na kufunga mpaka mambo yakakaa sawa, “Sasa hili la mtu kukutwa na mguu wa binadamu mwenzake, nalo limetuliza, Mungu apishie mbali jamani,” alisema mzee huyo.
George Mwangata, muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (chini ya Askofu Mkuu, Alex Malasusa) Soko Matola, jijini humu, alisema kitendo cha mtuhumiwa kukutwa na kiungo hicho ni pigo kwa makanisa, kwani Mbeya ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makanisa mengi nchini Tanzania.
Mama Nitike, muumini wa Roman Catholic (chini ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo), Mwanjelwa, Manispaa ya Mbeya, alisema alishtuka kusikia habari hizo na hajaamini kama kweli kiungo hicho kilikuwa ni cha binadamu.
“Kwa kweli sijaamini, he! Kweli binadamu unatembea na kiungo cha binadamu mwenzako, mh!” Alishangaa sana mama Nitike.
Aidha, Risasi Jumamosi lilipata bahati ya kuongea na Paulina Mwakifwamba, muumini wa Kanisa la Anglican (chini ya Askofu Costantine Mokiwa pichani), Rungwe ambapo alisema kuna haja ya umoja wa makanisa mkoani humo kukaa haraka na kufanya maombi ya kufunga siku tatu ili kumwomba Mungu aondoe roho inayotaka kuinuka, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Naye muumini wa kanisa la Full Gospel&Bible Fellowship (FGBF) ambalo lipo chini ya Askofu Mkuu, Zacharia Kakobe, aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank, tawi la Mbeya alisema maombi ya kufunga yanatakiwa kwa ajili ya mwelekeo mzima wa uchaguzi mkoani humo, mbali na suala la mgombea huyo kukutwa na mguu wa binadamu.
George Mtasha ni mgombea Ubunge jimbo jipya la Makongorosi, wilayani Chunya na mwenzake, Paul Mnyambwa, walikutwa na kiungo hicho saa 12.50 alfajiri ya Jumatano, Julai 21, 2010 na kushikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema, uchunguzi mkali unaendelea.
Wakiongea na Mwandishi Wetu, baadhi ya waumini hao walisema kuwa, wanaamini kitendo hicho ni ishara ya mwanzo wa vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikiukumba mkoa wa Mbeya miaka ya karibuni.
Josephat Mwaibabile ambaye ni Mzee wa Kanisa la Kiroho la Jerusalem Temple, alisema kuwa mkoa wa Mbeya una skendo ya watu kuchunwa ngozi, waumini wakalia kwa Mungu kwa maombi na kufunga mpaka mambo yakakaa sawa, “Sasa hili la mtu kukutwa na mguu wa binadamu mwenzake, nalo limetuliza, Mungu apishie mbali jamani,” alisema mzee huyo.
George Mwangata, muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (chini ya Askofu Mkuu, Alex Malasusa) Soko Matola, jijini humu, alisema kitendo cha mtuhumiwa kukutwa na kiungo hicho ni pigo kwa makanisa, kwani Mbeya ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makanisa mengi nchini Tanzania.
Mama Nitike, muumini wa Roman Catholic (chini ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo), Mwanjelwa, Manispaa ya Mbeya, alisema alishtuka kusikia habari hizo na hajaamini kama kweli kiungo hicho kilikuwa ni cha binadamu.
“Kwa kweli sijaamini, he! Kweli binadamu unatembea na kiungo cha binadamu mwenzako, mh!” Alishangaa sana mama Nitike.
Aidha, Risasi Jumamosi lilipata bahati ya kuongea na Paulina Mwakifwamba, muumini wa Kanisa la Anglican (chini ya Askofu Costantine Mokiwa pichani), Rungwe ambapo alisema kuna haja ya umoja wa makanisa mkoani humo kukaa haraka na kufanya maombi ya kufunga siku tatu ili kumwomba Mungu aondoe roho inayotaka kuinuka, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Naye muumini wa kanisa la Full Gospel&Bible Fellowship (FGBF) ambalo lipo chini ya Askofu Mkuu, Zacharia Kakobe, aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank, tawi la Mbeya alisema maombi ya kufunga yanatakiwa kwa ajili ya mwelekeo mzima wa uchaguzi mkoani humo, mbali na suala la mgombea huyo kukutwa na mguu wa binadamu.
George Mtasha ni mgombea Ubunge jimbo jipya la Makongorosi, wilayani Chunya na mwenzake, Paul Mnyambwa, walikutwa na kiungo hicho saa 12.50 alfajiri ya Jumatano, Julai 21, 2010 na kushikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema, uchunguzi mkali unaendelea.
Thursday, July 22, 2010
Wednesday, July 21, 2010
PIGO KUBWA KWA FAMILIA YA MR AGREY MWAMBUSI WA JIJINI MBEYA
Aliyekuwa mmiliki wa shule za St Agrey pamaja na chuo cha ualimu Agrey (Mr.Agrey Mwambusi) , alipata ajari alipo akiludi nyumbani kwake baada ya kutoka kwenye sherehe ndogo ya kumpongeza mwanawe Mr Mboka Mwabusi, kwa kuludi kwake salama kutoka Africa ya kusini aliko kwenda kushuhudia mechezo ya fainali za kombela dunia 2010 . katika ajali hii ime semekana kuwa watu wawili wali poteza maisha pale pale akiwemo mke wa marehemu Agrey Mwambusi ambaye amejeruhiwa vibaya sana

Tuesday, July 20, 2010
Presenting Top class art works
Hii ni blog mpya ambayo imejikita zaidi na art work za aina mbalimbali kutoka vijana wenye uwezo na kazi zenye kuvutia . www.topclassartworks.blogspot.com ndio link ya kuitazama nyote mnakalibishwa
Sunday, July 18, 2010
Waziri Mkuu Uhispania asusa kumwona Kagame

Uamuzi huu wa Bw Zapatero ulikuwa ni wa dakika za mwisho. Yeye mwenyewe hakuzungumzia suala hillo, ila naibu wake amesema waziri mkuu alipokea maombi kutoka kwa vyama kadhaa vya kisiasa vya Uhispania ili asikutane na Rais wa Rwanda.
Naibu waziri mkuu alisema Bw Zapatero aliyachukulia maombi hayo kwa uzito na kukubaliana nayo.
Kwa hivyo mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, ulihamishiwa kwenye hoteli, na Uhispania badala yake ikawakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeni.
Mgogoro huo wa kidiplomasia unahusiana na mashtaka dhidi ya Rais wa Rwanda yaliyoanzishwa na jaji mwandamizi wa Uhispania miaka miwili iliyopita.
Jaji huyo alitoa hati ya kukamatwa kwa wanajeshi 40 wa Rwanda, akiwashtumu kutekeleza mauaji makubwa ya kulipizia kisasi dhidi ya jamii wa Kihutu mwaka wa 1994, baada ya mauaji ya kimbari ya maelfu ya jamii ya Kitutsi.
Wanajeshi hao wakati huo walikuwa chini ya utawala wa Rais Kagame - lakini Kagame ni rais wa nchi na ana kinga ya kumlinda dhidi ya mashtaka.
Mwezi uliopita, kiongozi wa Rwanda aliteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza na Bw Zapatero wa kundi lenye majukumu ya kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya millenia.
Ban Ki Moon alimchagua Kagame kutokana na mchango wake wa mafanikio ya Rwanda katika kupunguza vifo vya watoto.
Bw Ban alisita kuzungumzia akiwa mjini Madrid madai ya mahakama hiyo ya Uhispania.
Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu Zapatero aliwapokea wageni wote wa mkutano huo ofisini kwake -isipokuwa Rais Kagame wa Rwanda.
BIG BROTHER All Stars LIVE KUTOKEA SOUTH AFRICA.
Nembo mpya ya inayotumika kwa mwaka huu
MC wa shughuli hii ingawa
Mwisho akiwa na mshiri mwingine Janet kutoka Mozambique
ONE INCREDIBLE.
Watu wengi walikuwa wananiuliza yule mshkaji anayeitwa One ameimba wimbo wa Incredible mbona hatumjui, jana bahati nzuri nilikutana nae maeneo ya Mzalendo Pub na tukapiga story nyingi tu kuhusiana na projct zake.
Sasa jamaa mwenyewe ndio huyo hapo kwenye picha, ni msanii wa bongo anayeimba Hip Hop iliyokwenda xcul na anafanya vizuri kwa kweli
Sasa jamaa mwenyewe ndio huyo hapo kwenye picha, ni msanii wa bongo anayeimba Hip Hop iliyokwenda xcul na anafanya vizuri kwa kweli
Dawa mpya ya kuzindua watu ICU.
Ukiangalia video ya wimbo wa robo saa wa Amini utaona mtu aliepoteza fahamu na juhudi zote za madaktari kumzindua zinashindikana mpaka anapokuja mpenzi wake na baada tu ya kumbusu jamaa anazinduka.Hii imenifanya nifikiri hamna haja ya kutumia mamilioni kwa dawa na mashine za kuzindua watu,tuajiri wavulana na wasichana warembo katika kila hospitali wawe wanazindua watu wanaopoteza fahamu.
Hizi ndizo awards ndani ya tamasha la filamu la Zanzibar
Golden Dhow - Best Feature Film - THEMBA by Stefanie Sycholt (South Africa)
Silver Dhow - Best Feature Film - IMANI by Caroline Kamya (Uganda)
Golden Dhow - Best East African Talent - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau Wa Ndung'u and Nick Reding (Kenya)
Golden Dhow - Best Short Film - THE GIFT by Jill Soong (Singapore)
Golden Dhow - Special Jury Prize - PUMZI by Wanuri Kahiu (Kenya)
Golden Dhow - Best Documentary - MOTHERLAND by Owen Alik Shahadah (UK)
VERONA AFRICAN FILM FESTIVAL AWARD
Winner - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau Wa Ndung'u and Nick Reding (Kenya)
SIGNIS AWARDS
Winner - SOUL BOY by Hawa Essuman (Kenya and Germany)
1st Commendation - A STEP INTO DARKNESS by Atil Inac (Turkey)
2 nd Commendation - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau wa Ngungu and Nick Reding (Kenya)
East African Talent Award - MY CITY ON FIRE by Dennis Onen (Uganda)
SEMBENE OUSMANE AWARD
Winner - SHUNGU by Saki Mafundikwa
1ST mention - THE GARDENER AND HIS 21 FLOWERS by Emil Lamgballe and Maria Samota le Dous
2ND mention - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau wa Ngungu and Nick Reding (Kenya)
UNICEF AWARD
Winner - THEMBA by Stefanie Sycholt (South Africa)
CHAIRMAN AWARD
Winner - MY POLICY by Phad Mutumba (Uganda/Canada)
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
Winner - Professor Jengo
BEST TANZANIAN FILM
Winner - NANI - by Sajni Srivastava
BEST ACTOR/ACTRESS
Winner - YVONNE CHERRY
Pichani kuna watu waliojumuika akiwemo naibu waziri wa habari wa zanzibar, Kombo na nyingine nilikuwa nakabidhi tuzo jirani yetu wa Kenya tuzo ya ZIFF ka afrika mashariki.
Subscribe to:
Posts (Atom)