Kuna ripoti zimetufikia kwamba super star aliyetisha katika movie kibao kama RUSH HOUR 1 2 na 3, pamoja na FRIDAY Actor Chriss Tucker anajaribu kulazimisha kuuza Jumba lake la kifahari alilolinunua miaka mitatu iliyopita, Inavyoonekana jamaa alitangaza dau kubwa, Ma Don wa kiwanja wakampotezea jumba hilo alili… Continue

Saturday, July 31, 2010
CHRISS TUCKER ANAUZA JUMBA LAKE KWA BEI CHEE
Kuna ripoti zimetufikia kwamba super star aliyetisha katika movie kibao kama RUSH HOUR 1 2 na 3, pamoja na FRIDAY Actor Chriss Tucker anajaribu kulazimisha kuuza Jumba lake la kifahari alilolinunua miaka mitatu iliyopita, Inavyoonekana jamaa alitangaza dau kubwa, Ma Don wa kiwanja wakampotezea jumba hilo alili… Continue
Kanye at FB - "Chain Heavy"/Freestyle?
Siku ya jumanne Rapper kanye West alitokeza makao makuu ya facebook nchini marekani na Kuperform mbele ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, Jamaa alikuwa katupia Suti nyeusi, show hiyo inavyoonekana haikuwa Rasmi kiviile koz hakukuwa na stage, so kanye alipanda juu ya meza za ofisi hiyo na Kuperform ngoma zake mpya zinazohisiwa zitakuwemo katika album yake anayoipika ndani ya mji wa Hawaii, Wachambuzi wa maasuala ya muziki wanasema huenda hatua hiyo ya Kanye west Kuperform mbe… Continue
Thursday, July 29, 2010
Wednesday, July 28, 2010
"HUU NI WARAKA WANGU KWA WASANII WA MZIKI KABLA YA UCHAGUZI MWEZI OCTOBER"
Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi october mwaka 2010,huu ni waraka wangu kwa wasanii wote wa mziki wa kibongo!. Najua kuna miaka mingi sana ya kuukomboa huu mziki wetu lakini wazungu wanasema "One step at a time"...na muda ndio huuu..........!!!!
Miaka kibaao sasa wasanii mmekuwa mkilalamika juu ya kudhulumiwa haki zenu kwa kuibiwa kazi zenu na kulipwa malipo madogo ya album zenu kiwango kisichokidhi mahitaji yenu,hilo ni sawa kabisaaa!!
LAKINI je!! mmejipanga vp kumaliza hili tatizo lenu? kila kukicha viongozi wanawa-ahidi kwa mdomo kuwa watamaliza tatizo lenu bila utekelezaji wa vitendo kitu ambacho mimi nakiona kama ni kiini macho na nyinyi wenyewe mnakifahamu....
Viongozi hawa hawa ambao wanakataa kwa "makusudi" kusimamia maslahi yenu ndio hao hao wanaokuwa wa kwanza kuwachukua nyinyi wakati wa uchaguzi ili muwasaidie kuwapigia kampeni kwa kutoa burudani pindi wanapokuwa kwenye mikutano yao,,,,
Sasa inakuwaje mnatumika kirahisi namna hii? wakati kwenye interview zenu wengi wenu mnajinadi kuwa nyinyi ni wanaharakati na sasa mnafanya mageuzi ya huu mziki wenu,vp mageuzi ndio haya? Mnapotumiwa kwenye kampeni mnacheka cheka kwa furaha pale mnapopewa laki kadhaa au vimilioni kama shukrani ya "kinafki" kutoka kwa hao watu waliowatumia!!!! Na baada ya kumaliza kampeni zao hao hao wakiwa madarakani wanawasahau na kujifanya hawawakumbuki tena hadi wakati mwingine wa uchaguzi.....(huu ni utumwa wa kifikra) najua mtasema mnaangalia pesa na ndio mana mnawafanyia kazi yao na sio kitu kingine!!! Sawa sikatai huenda ni kweli pesa ndio mnayofuata,,, sasa je? nyie wasanii wa kiume ikitokea wamama wakiwapa pesa za kutosha na kuwataka mkatumbuize kwenye "kitchen party" yao mtaenda kudhalilishwa sababu ya pesa au mtakataa?
Sidhani kama ntapata dhambi nikisema kuwa kitendo cha wasanii kutumiwa kwa muda na hawa watu mi nakifananisha na binti wa kike ambae bwana wake huwa anajifanya kumjali na kumfuata pale anapotaka penzi lake tu!! na akishamaliza shida zake anaondoka na kumuacha binti huyo akiteseka na hali ngumu ya maisha bila ya msaada wowote na hurudi tena pale anapokuwa na shida hiyo!!
Enyi wasanii kwanini mnajipa thamani ndogo kiasi hicho???
Huu ndio wakati wenu wasanii kuonesha mapinduzi yenu na misimamo yenu na zile harakati ambazo kila kukicha mmekuwa mkizitaja kwenye nyimbo zenu na interview zenu,,,yawapasa kudai maslahi yenu kwanza kuliko kutumika kuhangaikia maslahi ya watu wengine....
Sitoona ajabu nikiwaona wasanii wale wale wanaokuwa wa kwanza siku zote kudai haki zao wakitumika kwenye kampeni mwezi october na kisha baada ya uchaguzi mwakani wasanii hao hao tutawaskia tena wakilalamika kutokumbukwa na viongozi husika!!!
"CALCULATE THE RISK,BEFORE YOU JUMP"
Sunday, July 25, 2010
Fataki............ Umewahi kujiuliza haya?
atika kuwalinda wasichana dhidi ya KUDANGANYIKA na KUHARIBU NDOTO ZA MAISHA YAO... kuna matangazo kadhaa yanatoka kwenye redio na TV kuhusu "FATAKI".Hivi ndugu zanguni, pamoja na nia njema kabisa ya kutetea haki za watoto wa kike, mmeshawahi kujiuliza athari wazipatazo wakina kaka, baba wenye majina ya FATAKI, na vile vile watoto ambao baba zao wana majina ya FATAKI? Leo nilisikia kisa cha mtoto aliyetaka baba yake anayeitwa FATAKI abadili jina maana shuleni watoto wenzie wanamcheka! Baba naye akajaribu kumshari mwanae kuwa jina hilo lina historia ndefu sana katika ukoo na hawezi kubadili! Nikajiuliza, huyu mtoto naye si ana haki zake? Huko shule kama anataniwa ni dhahiri kuwa anapoteza kujiamini, ana athirika kisaikolojia na hatimaye athari hizi zina uwezekano kum haribia ndoto zake za maisha bora huko mbeleni.
Kwa haraka haraka, nikasema hili linahitaji mjadala mrefu ili kudadavua yaliyomo kama yamo ninavyoyaona mimi.
Karibuni tujadili ili tuwalinde wenye majina ya FATAKI na kutetea haki zao.
Kwa haraka haraka, nikasema hili linahitaji mjadala mrefu ili kudadavua yaliyomo kama yamo ninavyoyaona mimi.
Karibuni tujadili ili tuwalinde wenye majina ya FATAKI na kutetea haki zao.
Mbunge mtarajiwa kupitia Chadema aliyenaswa na mguu wa mtu aliza makanisa
Baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali mkoani hapa, wako katika kilio kufuatia kitendo cha mgombea Ubunge wa Chadema aliyerudisha fomu, George Mtasha (50) kudakwa na jeshi la Polisi wilayani Chunya akiwa na mguu wa kushoto wa binadamu, Risasi Jumamosi linashuka kikamilifu.
Wakiongea na Mwandishi Wetu, baadhi ya waumini hao walisema kuwa, wanaamini kitendo hicho ni ishara ya mwanzo wa vitendo viovu ambavyo vimekuwa vikiukumba mkoa wa Mbeya miaka ya karibuni.
Josephat Mwaibabile ambaye ni Mzee wa Kanisa la Kiroho la Jerusalem Temple, alisema kuwa mkoa wa Mbeya una skendo ya watu kuchunwa ngozi, waumini wakalia kwa Mungu kwa maombi na kufunga mpaka mambo yakakaa sawa, “Sasa hili la mtu kukutwa na mguu wa binadamu mwenzake, nalo limetuliza, Mungu apishie mbali jamani,” alisema mzee huyo.
George Mwangata, muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (chini ya Askofu Mkuu, Alex Malasusa) Soko Matola, jijini humu, alisema kitendo cha mtuhumiwa kukutwa na kiungo hicho ni pigo kwa makanisa, kwani Mbeya ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuwa na makanisa mengi nchini Tanzania.
Mama Nitike, muumini wa Roman Catholic (chini ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo), Mwanjelwa, Manispaa ya Mbeya, alisema alishtuka kusikia habari hizo na hajaamini kama kweli kiungo hicho kilikuwa ni cha binadamu.
“Kwa kweli sijaamini, he! Kweli binadamu unatembea na kiungo cha binadamu mwenzako, mh!” Alishangaa sana mama Nitike.
Aidha, Risasi Jumamosi lilipata bahati ya kuongea na Paulina Mwakifwamba, muumini wa Kanisa la Anglican (chini ya Askofu Costantine Mokiwa pichani), Rungwe ambapo alisema kuna haja ya umoja wa makanisa mkoani humo kukaa haraka na kufanya maombi ya kufunga siku tatu ili kumwomba Mungu aondoe roho inayotaka kuinuka, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010.
Naye muumini wa kanisa la Full Gospel&Bible Fellowship (FGBF) ambalo lipo chini ya Askofu Mkuu, Zacharia Kakobe, aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank, tawi la Mbeya alisema maombi ya kufunga yanatakiwa kwa ajili ya mwelekeo mzima wa uchaguzi mkoani humo, mbali na suala la mgombea huyo kukutwa na mguu wa binadamu.
George Mtasha ni mgombea Ubunge jimbo jipya la Makongorosi, wilayani Chunya na mwenzake, Paul Mnyambwa, walikutwa na kiungo hicho saa 12.50 alfajiri ya Jumatano, Julai 21, 2010 na kushikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Advocate Nyombi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema, uchunguzi mkali unaendelea.

Thursday, July 22, 2010
Wednesday, July 21, 2010
PIGO KUBWA KWA FAMILIA YA MR AGREY MWAMBUSI WA JIJINI MBEYA
Aliyekuwa mmiliki wa shule za St Agrey pamaja na chuo cha ualimu Agrey (Mr.Agrey Mwambusi) , alipata ajari alipo akiludi nyumbani kwake baada ya kutoka kwenye sherehe ndogo ya kumpongeza mwanawe Mr Mboka Mwabusi, kwa kuludi kwake salama kutoka Africa ya kusini aliko kwenda kushuhudia mechezo ya fainali za kombela dunia 2010 . katika ajali hii ime semekana kuwa watu wawili wali poteza maisha pale pale akiwemo mke wa marehemu Agrey Mwambusi ambaye amejeruhiwa vibaya sana

Tuesday, July 20, 2010
Presenting Top class art works
Hii ni blog mpya ambayo imejikita zaidi na art work za aina mbalimbali kutoka vijana wenye uwezo na kazi zenye kuvutia . www.topclassartworks.blogspot.com ndio link ya kuitazama nyote mnakalibishwa
Sunday, July 18, 2010
Waziri Mkuu Uhispania asusa kumwona Kagame

Uamuzi huu wa Bw Zapatero ulikuwa ni wa dakika za mwisho. Yeye mwenyewe hakuzungumzia suala hillo, ila naibu wake amesema waziri mkuu alipokea maombi kutoka kwa vyama kadhaa vya kisiasa vya Uhispania ili asikutane na Rais wa Rwanda.
Naibu waziri mkuu alisema Bw Zapatero aliyachukulia maombi hayo kwa uzito na kukubaliana nayo.
Kwa hivyo mkutano huo ambao ulifadhiliwa na Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, ulihamishiwa kwenye hoteli, na Uhispania badala yake ikawakilishwa na waziri wake wa mambo ya kigeni.
Mgogoro huo wa kidiplomasia unahusiana na mashtaka dhidi ya Rais wa Rwanda yaliyoanzishwa na jaji mwandamizi wa Uhispania miaka miwili iliyopita.
Jaji huyo alitoa hati ya kukamatwa kwa wanajeshi 40 wa Rwanda, akiwashtumu kutekeleza mauaji makubwa ya kulipizia kisasi dhidi ya jamii wa Kihutu mwaka wa 1994, baada ya mauaji ya kimbari ya maelfu ya jamii ya Kitutsi.
Wanajeshi hao wakati huo walikuwa chini ya utawala wa Rais Kagame - lakini Kagame ni rais wa nchi na ana kinga ya kumlinda dhidi ya mashtaka.
Mwezi uliopita, kiongozi wa Rwanda aliteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza na Bw Zapatero wa kundi lenye majukumu ya kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya millenia.
Ban Ki Moon alimchagua Kagame kutokana na mchango wake wa mafanikio ya Rwanda katika kupunguza vifo vya watoto.
Bw Ban alisita kuzungumzia akiwa mjini Madrid madai ya mahakama hiyo ya Uhispania.
Siku ya Ijumaa, Waziri Mkuu Zapatero aliwapokea wageni wote wa mkutano huo ofisini kwake -isipokuwa Rais Kagame wa Rwanda.
BIG BROTHER All Stars LIVE KUTOKEA SOUTH AFRICA.
Nembo mpya ya inayotumika kwa mwaka huu
MC wa shughuli hii ingawa
Mwisho akiwa na mshiri mwingine Janet kutoka Mozambique
ONE INCREDIBLE.
Watu wengi walikuwa wananiuliza yule mshkaji anayeitwa One ameimba wimbo wa Incredible mbona hatumjui, jana bahati nzuri nilikutana nae maeneo ya Mzalendo Pub na tukapiga story nyingi tu kuhusiana na projct zake.
Sasa jamaa mwenyewe ndio huyo hapo kwenye picha, ni msanii wa bongo anayeimba Hip Hop iliyokwenda xcul na anafanya vizuri kwa kweli
Sasa jamaa mwenyewe ndio huyo hapo kwenye picha, ni msanii wa bongo anayeimba Hip Hop iliyokwenda xcul na anafanya vizuri kwa kweli
Dawa mpya ya kuzindua watu ICU.
Ukiangalia video ya wimbo wa robo saa wa Amini utaona mtu aliepoteza fahamu na juhudi zote za madaktari kumzindua zinashindikana mpaka anapokuja mpenzi wake na baada tu ya kumbusu jamaa anazinduka.Hii imenifanya nifikiri hamna haja ya kutumia mamilioni kwa dawa na mashine za kuzindua watu,tuajiri wavulana na wasichana warembo katika kila hospitali wawe wanazindua watu wanaopoteza fahamu.
Hizi ndizo awards ndani ya tamasha la filamu la Zanzibar
Golden Dhow - Best Feature Film - THEMBA by Stefanie Sycholt (South Africa)
Silver Dhow - Best Feature Film - IMANI by Caroline Kamya (Uganda)
Golden Dhow - Best East African Talent - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau Wa Ndung'u and Nick Reding (Kenya)
Golden Dhow - Best Short Film - THE GIFT by Jill Soong (Singapore)
Golden Dhow - Special Jury Prize - PUMZI by Wanuri Kahiu (Kenya)
Golden Dhow - Best Documentary - MOTHERLAND by Owen Alik Shahadah (UK)
VERONA AFRICAN FILM FESTIVAL AWARD
Winner - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau Wa Ndung'u and Nick Reding (Kenya)
SIGNIS AWARDS
Winner - SOUL BOY by Hawa Essuman (Kenya and Germany)
1st Commendation - A STEP INTO DARKNESS by Atil Inac (Turkey)
2 nd Commendation - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau wa Ngungu and Nick Reding (Kenya)
East African Talent Award - MY CITY ON FIRE by Dennis Onen (Uganda)
SEMBENE OUSMANE AWARD
Winner - SHUNGU by Saki Mafundikwa
1ST mention - THE GARDENER AND HIS 21 FLOWERS by Emil Lamgballe and Maria Samota le Dous
2ND mention - NDOTO ZA ELIBIDI by Kamau wa Ngungu and Nick Reding (Kenya)
UNICEF AWARD
Winner - THEMBA by Stefanie Sycholt (South Africa)
CHAIRMAN AWARD
Winner - MY POLICY by Phad Mutumba (Uganda/Canada)
LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD
Winner - Professor Jengo
BEST TANZANIAN FILM
Winner - NANI - by Sajni Srivastava
BEST ACTOR/ACTRESS
Winner - YVONNE CHERRY
Pichani kuna watu waliojumuika akiwemo naibu waziri wa habari wa zanzibar, Kombo na nyingine nilikuwa nakabidhi tuzo jirani yetu wa Kenya tuzo ya ZIFF ka afrika mashariki.
Subscribe to:
Posts (Atom)