

Monday, November 23, 2009
Wednesday, November 18, 2009
MO RACKA AJITOA RACKAS

Muasisi na muanzilishi wa kundi la RACKAS ( RACKA'S FAMILY ) linalo undwa na wasaani kama quick racka, chief racka na dowracka pammojana Mo racka ambaye amejitoa katika kundi hilo kwa sababu ambazo yeye mwenyewe hakuzisema.Morraca amesema amejitoa kundini lakini sababu atazifafanua zaidi sio muda mrefu.utapata updates mara tu taarifa zitakaponifikia
Friday, November 13, 2009
HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA KWENYE SHOW YA WAHAPAHAPA
Hiki ndio choo cha mbuyu bwana

Mbuyu umekuwa ukitumiwa kama makazi na makabila mengi yanayoishi sehemu kame ambako ndiko hasa mmea huu unastawi vizuri mf. Watindiga na Wafulani. Kuweka choo cha kisasa ndaniye ni kupanua tu matumizi yake ya tangu zamani ingawa si ajabu watu wanaotetea mazingira wakadai kwamba kitendo kama hiki cha kuugeuza mbuyu kuwa choo si kitendo cha kujivunia kwani kinahatarisha maisha yake.

Mimi sivuti na lengo langu hapa siyo kuwatetea wavuta sigara. Wanasayansi wameshathibitisha kwamba uvutaji wa sigara ni tabia ya hatari inayoua mamilioni ya watu kila mwaka kutokana na saratani ya mapafu na magonjwa mengine yanayoathiri mfumo wa upumuaji. Kutokana na sababu hii uvutaji wa sigara umepigwa marufuku karibu katika kila kona ya dunia. Sehemu zingine zimefikia hatua ya kutunga sheria zinazowabana wavuta sigara kutovuta hata wakiwa majumbani mwao. Mwezi uliopita chuo kikuu cha Florida kilipitisha sheria ambayo inapiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo yote ya chuo – ndani na nje. Sijui wavuta sigara watafanyeje!
Swali langu ni hili: mbona tumekomalia sana sigara utafikiri kwamba uvutaji ndiyo tabia pekee-angamizi? Mbona tabia zingine za hatari kama unywaji wa bia (ambao pia, mbali na matatizo mengine, umeshathibitishwa kuwa kisababishi kimojawapo kikuu cha aina mbalimbali za saratani na hasa zile za matumbo) hatuzikomalii kama uvutaji sigara? Vipi kuhusu ulaji wa nyama hasa zile “nyekundu” ambao nao pia umeshathibitishwa kwamba ni hatari kwa afya? Wavuta sigara wanaonewa?
Mimi ni mmoja kati ya watu wasiopenda tabia za kinafiki za kujifanya kuchukia tabia moja angamizi na kukumbatia zingine za aina hiyo hiyo. Ndiyo maana huwa sielewi mtu anaponiambia eti ameamua kuacha kula nyama ili kulinda afya yake na wakati huo huo anazitandika bia sawasawa, kuvuta sigara na hata kuwa “kiwembe”.
Ni mawazo yangu tu. Pengine mwanafalsafa Kitururu angeweza kusema ninachojaribu kukisema hapa kwa ufasaha zaidi!
Wasikilize watafiti hapa wakijadili athari za ulaji wa nyama, uvutaji wa sigara na unene wa futufutu (obesity) kwa afya.
Thursday, November 12, 2009
HASHEEM THABIT AVUNJIKA TAYA

Mchezaji wa kati wa timu ya Memphis Grizzlies Hasheem Thabeet amevunjika taya lake la chini siku ya jana, alipokuwa akichezea na timu yake wakiminyana na Portland Trail Blazers, mchezo amabo ulimalizika kwa Blazers kutoka na ushindi wa pointi 93 kwa 79.
Hii sasa inamaanisha kuwa Hasheem hatokuwemo kwenye msafara wa timu yake ya Grizzlies itakapokuwa ikienda kucheza na Houston Rockets usiku wa leo.
Hata hivyo habari si mbaya sana za kuumia kwake kwani baada ya uchunguzi wa madaktari imefahamika kuwa, hatohitaji upasuaji, ili kutibu maumivu na wakasema anatarajiwa awe amepona si muda mrefu sana kuanzia sasa
Subscribe to:
Posts (Atom)