Tuesday, February 2, 2010

Padri akamatwa kwa wizi


  • Steven Poole, padri wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 41 amekamatwa kwa kuiba siagi pamoja na kitambaa cha kufunikia makochi katika duka kubwa la Wal-Mart kule Illinois nchini Marekani. Padri huyo alishindwa kulipia kopo la siagi lenye thamani ya dola 3.22 na kitambaa cha kufunikia makochi chenye thamani ya dola 60.00 katika kituo cha kulipia ambacho hakisimamiwi na karani au keshia. Padri huyo alitenda kosa hilo tarehe 25/1/2010.
  • Baada ya kufanikiwa kuiba vitu hivyo, padri huyo alirudi tena katika duka hilo kubwa, akachukua godoro moja spesheli kisha akabadilisha lebo ya bei. Thamani ya godoro hilo maalum ilikuwa ni dola 145 lakini padri huyo alibadilisha bei hiyo na kumfanya alipe dola 31 tu.
Mtumishi huyu wa Mungu pia alikutwa na vifaa vya kompyuta ya mkononi ambavyo polisi wanadai kwamba ni vya wizi. Kutokana na kasheshe hili, polisi wamemfungulia mashtaka mawili ya wizi na yuko nje kwa dhamana. Kwa habari zaidi kuhusu kisa hiki

No comments:

Post a Comment