
Saturday, December 25, 2010
Weakleaks Yaihusisha Tanzania Na Uranium DRC
BAADA ya tovuti inayovujisha siri nyeti za Serikali za nchi mbalimbali duniani kuanika siri za Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mtandao huo wa WeakLeaks umefichua siri nyingine nzito kudai kuwa Tanzania ni kitovu cha
usafirishaji madini ya uranium kwenda nchini Iran
Kwa mujibu wa taarifa za tovuti hiyo, Marekani inazishutumu nchi mbili katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania kwa kwa madai ya kuwa kitovu cha usafirishaji kinyemela madini hayo hatari.
WeakLeakes ambao ulifichua siri mbalimbali za Balozi za Marekani, unaitaja Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuwa ndilo chimbuko la madini hayo ambayo baada ya kusafishwa hutumika kutengeneza nguvu ya umeme na silaha hatari.
Ilidaiwa kuwa madini hayo ya uranium yanachimbwa na kampuni za kigeni katika Jimbo la Katanga kabla ya kampuni hizo kuyasafirisha kwenda Iran kupitia ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika taarifa za mtandao huo, mwanadiplomasia wa Marekani jijini Dar es Salaam, Purnell Delly Septemba 2006 anadaiwa kuripoti kwa wakuu wake mjini Washington akisema inafahamika wazi meli zilizosheheni madini ya uranium zimekuwa zikipita katika bandari ya Dar es Salaam zikiwa njiani kwenda Iran.
Kutokana na taarifa hiyo miaka miwili baadaye Polisi wa Kenya waliamua kuingilia kati kile walichohisi, Uganda kusafirisha madini hayo kutoka DRC na kufanikiwa kukamata vifaa hatari vya milipuko na kutiwa mbaroni wanaume wawili waliodaiwa kununu vitu hivyo kutoka DRC kwa thamani ya sh. milioni 3.9 na walipanga kuviuza mjini Nairobi kwa thamani ya sh. milioni Sh.100.
Mei mwaka huu, Polisi nchini Kenya walifanikiwa kukamata kilo 10 ya vitu vinavyosadikika kuwa ni madini ya uranium, hali ambayo ilizua taharuki kwa Jumuiya za Kimataifa kwamba nchi hiyo ilikuwa ikitumika kama njia ya kusafirishia madini hayo kutoka DRC.
Mtandao huo pia ulimnukuu Balozi wa Uswiss akidai kuwa Afrika Mashariki ndiyo njia kuu ya kusafisha madini ya Uranium.
“Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mwandamizi wa Uswiss, usafirishaji wa uranium kupitia bandari ya Dar es Salaam unafahamika bayana kati ya kampuni mbili za meli kutoka Uswiss,” aliandika Delly.
“Hans Peter Schoni,ambaye ni Balozi wa Uswiss nchini Tanzania, alishazungumzia kuhusu tuhuma za madini ya uranium kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kupitishwa katika nchi za Zambia na Tanzania kwenda Iran, lakini hakupewa jibu lolote kutoka kwa kampuni husika ama mahali panapodaiwa kupelekwa madini hayo,”aliongeza mwanadipolimasia huyo.
Alielezea kusikitishwa kwake pamoja na taasisi husika lakini haijawahi kuthibitishwa ama kukanushwa ripoti hizo kuhusu meli hizo za uranium.
Katika ripoti hiyo, Delly ana wasiwasi kwamba huenda mwanadiplomasia wa Marekani mjini Kinshasa, Dpopovich Econoff, ambaye tovuti hiyo ya siri ilimtaja Novemba mwaka 2007 akisema kuwa kuna madini mengi ya uranium nchini DRC.
“Haifahamiki wazi kama kampuni ya Malta Forest ama kampuni nyinginezo zilizopo katika Jimbo la Katanga zinahusika na usafirishaji wa uranium. Mazingira ya kuwepo kwa biashara hiyo yanaonekana lakini ushahidi wa uhakika ndiyo hauonekani,”aliripoti Econoff na kuongeza;
“Vilevile kuna faida kubwa kutokana na kiwango cha uranium kinachozalishwa na kampuni ya Malta Forest's Mines hususani tangu bei ya madini hayo ilipopanda kutoka wastani wa dola 15 mwaka 2004 na kufikia wastani wa dola 135 kwa paundi mwaka 2007,”
Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo madini hayo yanachimbwa kwa wingi na kampuni zinazomilikiwa na vigogo ndani ya Serikali ya DRC na kusafirishwa nje ya nchi kwa njia ya panya na mitandao ya rushwa.
Alisema mfano kampuni ya Malta Forest inahusishwa na mshauri wa Rais Joseph Kabila huku kampuni za Uswiss na Finnland zikijipatia faida kubwa kutokana na madini hayo katika Jimbo la Katanga. Chanzo, gazeti Majira
Thursday, December 2, 2010
SOKO KUU LA UHINDINI JIJINI MBEYA LA TEKETEA KWA MOTO
Wafanya biashara wakijaribu kuokoa mali zao kutoka madukani mwao
Umati mkubwa ulio jitokeza kushuhudio tukio la moto
Wafanya biashara wakikusanya vitu vidogovidogo vilivyo salia katika maduka yao
Moto ukiendelea kuteketeza soko kuu la uhindini
Wanahabari kutoka jijini Mbeya waki muhoji mmoja kati ya askari wa kikosi cha zima moto
Gari la kikosi cha zima moto likifika katika eneo la tukio kwa kuchelewa na baada ya muda kidogo kuondoka kwenda kujaza maji kwa madai kuwa maji yamekwisha
Subscribe to:
Posts (Atom)